SIMBA SC KUWEKA KAMBI YAKE MISRI

KIKOSI cha Simba SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids kwa maandalizi ya msimu wa 2025/26 kitaweka kambi nchini Misri.

Ikumbukwe kwamba leo Julai 29 2025 Simba SC inatarajiwa kutangaza mdhamini mpya na ratiba nzima ya maandalizi kuelekea msimu wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Kuna wachezaji wapya ambao watatambulishwa hivi karibuni ndani ya kikosi cha Simba SC na wengine watauzwa kutokana na kupata ofa kubwa.

Miongoni mwa majina ya wachezaji ambao wanatajwa kuwa watauzwa ni Che Malone ambaye ni beki huku kiungo Jean Ahoua naye inaelezwa kuwa kuna timu ambazo zinahitaji saini yake.

Julai 30 2025 kikosi cha Simba SC kinatarajiwa kukwea pipa kueleka Ismailia, Misri kwa ajili ya kambi hiyo. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 iliweka kambi pia Misri.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.