MDHAMINI MPYA SIMBA SC BETWAY MKATABA WAKE THAMANI NI BILIONI 20

MTENDAJI Mkuu wa Simba SC, Zubeda Sakuru amesema kuwa mkataba ambao wameingia na wadhamini wapya ambao ni BetWay unakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu Tanzania kutokana na thamani iliyopo kwenye mkataba huo wa miaka mitatu.

“Mkataba ambao tumeingia unakwenda kuleta mapinduzi kwenye mchezo wa soka hapa Tanzania na unakwenda kuongezea nguvu dhamira ya Simba kuwa klabu namba moja barani Afrika.

“Udhamini huu ambao thamani yake ni Bilioni 20 kwa miaka mitatu, unaonyesha namna Simba imedhamiria kuleta mabadiliko ya kuwa klabu kubwa,”.

Ni Julai 29 2025 Simba SC imetangaza jambo hili kubwa kwa Watanzania na mashabiki wa Simba SC ambayo itakwenda kuweka kambi Misri.

Msafara wa Simba SC unatarajiwa kukwea pipa Julai 30 2025 kwa ajili ya ziara maalumu ambayo ni kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2025/26. Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 Simba SC mdhamini wake mkuu alikuwa ni M Bet.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.