AZAM FC YAANZA MATIZI, IBENGE ATUMA UJUMBE

MATAJIRI wa Dar, Azam FC wameanza maandalizi kuelekea msimu wa 2025/26 chini ya Kocha Mkuu, Florent Ibenge.

Azam FC iligotea nafasi ya pili kwenye msimamo msimu wa 2024/25 na kiungo Feisal Salum alikuwa namba moja kwa kutengeneza pasi za mwisho ambazo ni 13 na alifunga mabao manne yote kwa mguu wa kulia.

Ibenge ameweka wazi kuwa ameona namna vijana wapya waliopo kwenye kikosi hicho wakiwa na ari kwenye mwanzo wa maandalizi ya msimu mpya jambo ambalo linampa matumaini kufanya vizuri msimu mpya.

“Tumeanza maandalizi na ninaona wachezaji wapya wakiwa na kitu ambacho kinawasukuma kwenye mazoezi na hii inatupa picha ya kuwa imara kwa msimu mpya na tupo tayari.”

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo ndani ya Azam FC kwa sasa ni Sopu, Sospeter Bajana huku Fei Toto akiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania ambayo ipo kwenye maandalizi kuelekea CHAN na Agosti 2 2025 itacheza mchezo dhidi ya Burkina Faso.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.