ROMAIN Folz kocha mpya wa Yanga SC ana balaa zito akiwa ni kocha kijana. Kocha huyo ni mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga SC 2024/25. Miloud alipewa Thank You Julai 3 2025 hivyo hatakuwa ndani ya Yanga SC msimu wa 2025/26 amepata changamoto mpya Klabu ya Ismaily SC ya Misri.
Ni Julai 23 Kocha Mkuu Romain Folz alitambulishwa Yanga SC. Rekodi zinaonyesha kuwa ni kocha ambaye amefundisha timu mbalimbali. Atakuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC ambacho kinaendelea na usajili wa wachezaji wapya. Wapo wengine ambao wataongeza kandarasi zao.
Timu ambazo alifundisha Romain hizi hapa:-
Kuhusu kocha mpya wa Yanga SC, mchambuzi Hans Rafael alibainisha kuwa ni miongoni mwa makocha bora. Hans alisema ana uzoefu na mashindano makubwa na alianza kazi akiwa kijana mdogo. Baada ya utambulisho wake alisema namna hii:
“Anaitwa Romain Folz (35) kocha mpya wa Yanga SC. Alizaliwa Bordeaux, Ufaransa. Huyu kocha amefanya kazi sehemu zifuatazo: -2025 alikuwa mkurugenzi wa michezo wa Olympique Akbou ya Algeria. 2024 alikuwa kocha msaidizi wa Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini.
“2023 alikuwa Kocha Mkuu wa Horoya ya Guinea. 2022 alikuwa Kocha Mkuu wa Amazulu ya Afrika ya Kusini. 2021 alikuwa Kocha Mkuu wa Township Rollers ya Botswana. 2019 alikuwa kocha msaidizi wa Pyramid ya Misri. 2018 alikuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Uganda.
“Huyu kocha ana UEFA Pro Licence na Pro Licence ya CONMEBOL (America). Huyu kocha ni muumini wa (4-3-3) na timu yake ina-press kinoma. Wananchi Remember the Name Romain Folz, balaa jingine ndani ya NBC Premier League,”.