YANGA SC YAMALIZANA NA MASHINE YA MABAO

YANGA SC hawana jambo dogo mara baada ya kumalizana na mashine ya mabao ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhamiwaniwa na NBC. Msimu wa 2024/25 nyota huyo alikuwa kwenye ubora akiwa ni chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Tabora United.

Ni Kiungo mshambuliaji aliyekuwa Tabora United, Offen Chikola alitambulishwa Yanga SC Julai 22 2025 kwa kandarasi ya miaka miwili.2024/25 akiwa na Tabora United alifunga mabao 8 kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo. Ni nafasi ya tano kwenye msimamo pointi 38 baada ya mechi 30 ilikusanya Tabora United.

Ipo wazi katika mchezo wa mzunguko wa kwanza, Uwanja wa Azam Complex 1-3 Yanga SC, Novemba 7 2024 mwamuzi alikuwa Nassoro Mwinchui. Chikola alifunga bao dakika ya 19 kwa mguu wa kushoto akitumia pasi ya Yacouba akiwa nje ya 18 na dakika ya 45 alifunga bao la pili kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18.

Dakika ya 77 ni Nelson Lunganga kwa mguu wa kulia akiwa ndani ya 18. Bao pekee la kufuta machozi kwa Yanga SC lilifungwa na Clement Mzize dakika ya 90 kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18 akitumia pasi ya Prince Dube.

Aziz Ki alikosa penati iliyosababishwa na Andy Bikoko baada ya kumchezea faulo Pacome. Kwenye mchezo huo dakika ya 45 Hussen Masalanga aliyeanza langoni alionyeshwa kadi ya njano kwa tafsri yakupoteza muda na kipa huyo aliokoa mkwaju wa penati ya Aziz Ki.

Nyota wa mchezo alikuwa ni Chikola ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo na Yanga SC ikipishana na pointi tatu mazima kwenye mchezo huo zama za Miguel Gamondi ambaye kwa msimu wa 2025/26 atakuwa ndani ya Singida Black Stars.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi