INAELEZWA kuwa baada ya Yanga SC kukamilisha usajili wa beki wa kushoto na nahodha wa Simba SC msimu wa 2024/25, Mohamed Hussein Zimbwe Jr wapo kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la mshambuliaji wa kazi.
Mshambuliaji huyo huenda akajiunga na Yanga SC kwa mkopo kwa makubaliano ya pande zote mbili ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu wa 2025/26.
Ipo wazi kwamba tayari Yanga SC ilimtambulisha mchezaji wao wa kwanza ambaye ni Balla Conte siku ya Ijumaa, sasa uongozi wa timu hiyo unakamilisha taratibu kumalizana na Sekhukhune United ya Afrika kusini kupata saini ya Andy Boyeli.
Yanga wamekamilisha usajili wa mshambuliaji Andy Bobwa Boyeli mwenye umri wa miaka 24 kutoka Sekhukhune United ya Afrika Kusini kwa mkopo wa kipindi cha msimu mmoja ambao una kipengele cha mchezaji huyo kununuliwa jumlajumla kwa gharama ya dola 100,000.
Staa huyo alikuwa na wakati mzuri msimu wa 2022/23 akiwa na kikosi cha Power Dynamos ya Zambia, ambapo Boyeli alifanikiwa kutwaa kiatu cha mfungaji bora wa ligi ya Zambia baada ya kufunga magoli 18. Kufuatia mafanikio hayo mwishoni mwa msimu nyota huyo alifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu (MVP).
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.