Klabu ya Yanga Sc imethibitisha kiungo Mudathir Yahya amesaini nyongeza ya mkataba mpya wa miaka miwili utakaombakisha klabuni hapo mpaka Juni 2027.
Mkataba wa awali wa Mudathir aliyejiunga na Wananchi mnamo Januari 2023 akitokea Azam Fc ulitamatika mwishoni mwa msimu uliomalizika lakini sasa amemwaga wino wa kuendelea kuitisha simu mitaa ya Jangwani kwa misimu miwili zaidi.