CHE MALONE KUONDOKA BONGO, TIMU HII YATAJWA

BEKI wa kati wa Simba raia wa Cameroon, Che Malone leo Jumanne Julai 22 anatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Algeria kwa ajili ya kukamilisha dili la usajili Klabu ya USM Alger.

Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo huenda hatakuwa sehemu ya kikosi cha Simba SC msimu wa 2025/26 kutokana na mabosi wa timu hiyo kufikiria maamuzi ya kumuuza.

Mcameroon huyo atajiunga na USM Alger, kama mazungumzo yatafikia hatua nzuri na Simba SC ambao ni mabosi wake kwa sasa.

Ni kandarasi ya mwaka mmoja imesalia ndani ya kikosi cha Simba SC hivyo dili likikwama huenda akarejea kuendelea na majukumu yake ndani ya kikosi cha Simba SC.

Kwa msimu wa 2024/25 Simba SC upande wa ulinzi ni timu namba mbili ambayo ilifungwa mabao machache ambayo ni 13 baada ya mechi 30 namba moja ni mabingwa Yanga SC ambao walifungwa mabao 10 baada ya mechi 30 ambazo ni dakika 2,700.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.