
LAMINE YAMAL AONGEZA MKATABA NA BARÇA HADI 2031, AKABIDHIWA JEZI NAMBARI 10 YA HESHIMA
Kinda mahiri wa FC Barcelona, Lamine Yamal, ametia saini mkataba mpya wa muda mrefu na klabu hiyo, ambao utamuweka Camp Nou hadi tarehe 30 Juni 2031. Tangazo hilo lilifanywa rasmi na Barcelona leo Jumanne, na limeambatana na hatua ya kihistoria ambapo Yamal amekabidhiwa rasmi jezi namba 10, namba yenye heshima kubwa katika historia ya klabu…