ZIJUE TIMU AMBAZO ZILIFUNGWA NA PACOME LIGI KUU/ MABAO 12

PACOME Zouzoua ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara amefunga mabao 12 akitoa jumla ya pasi 10 za mabao kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga SC iliyotwaa ubingwa wa ligi msimu wa 2024/25.

Hizi hapa timu ambazo zilifungwa na Pacome namna hii:-

JKT Tanzania, mchezo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex kwa mguu wake wa kushoto. Mchezo huu ulichezwa Oktoba 22 alitumia pasi ya Clatous Chama aliyempa kwa mguu wa kulia akiwa nje ya 18. Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania.

Namungo FC aliwafunga bao moja mzunguko wa kwanza. Ilikuwa Novemba 30 2024. Fountain Gate aliwafunga mabao mawili, Uwanja wa KMC Complex.

Singida Black Stars aliwafunga bao moja, Uwanja wa New Amaan Complex. Kagera Sugar aliwafunga bao moja kwa mkwaju wa penati dakika ya 77, Uwanja wa KMC Complex.

KenGold aliwafunga bao moja Uwanja wa KMC Complex. Bao pekee la kichwa alifunga kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union. Ni dakika ya 32 alipachika bao hilo katika mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex, Aprili 7 2025.

Alifunga bao moja mbele ya Azam FC. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90 ilikuwa Azam FC 1-2 Yanga SC. Mabao mawili alifunga kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Sokoine.

Bao la 12 alifikisha kwa kufunga mbele ya Simba SC. Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Juni 25 2025. Yanga SC ilisepa na pointi zote tatu mbele ya Simba SC.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.