SHOMARI Kapombe beki wakupanda na kushuka ndani ya kikosi cha Simba SC mkataba wake umegota mwisho na hajaongeza mkataba mwingine huku ikielezwa kuwa huenda akaondoka.
Kapombe ndani ya kikosi cha Simba SC kwenye mechi 30 ambazo ni dakika 2,700 alicheza mechi 27 akaikomba dakika 2,095.
Katika mabao 69 ambayo Simba SC imefunga kahusika kwenye mabao sita, kafunga mabao matatu na katengeneza jumla ya pasi tatu za mabao. Katika mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania alisababisha penati dakika ya 90 ilifungwa na Jean Ahoua.
Kapombe timu ambayo anaweza kwenda kucheza kwa Bongo asilimia kubwa ni Azam FC ambayo imemrejesha nyumbani kipa namba moja Aishi Manula.
Nyota huyo kwa sasa ameomba kuongezewa fedha kwenye upande wa mkataba wake na mshahara ili kuwa bora jambo ambalo linaleta mvutano na mabosi wa Simba SC.
Inaelezwa kuwa kazi ipo kwa sasa kwa mabosi wa Simba SC kuzungumza na mchezaji huyo ili asalie ndani ya Msimbazi kwa msimu wa 2025/26.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.