FEISAL Salum kiungo mshambuliaji wa Azam FC kuna asilimia ndogo kuondoka kwenye viunga hivyo kutokana na dau ambalo mabosi wamemuongezea kuelekea msimu wa 2025/25.
Taarifa zilikuwa zinaeleza kuwa kiungo huyo asilimia kubwa ataondoka hapo na timu ambayo ilikuwa inatajwa kwa ukaribu ilikuwa ni Simba SC.
Mkataba wake na Azam FC ni mwaka mmoja umebaki hivyo atautumia wote kuwa hapo msimu ujao. Simba SC inatajwa kuwa jitihada za kumpata mchezaji huyo zimegonga mwamba.
Rekodi zinaonyesha kuwa Feisal ni kiungo namba moja kwenye kutengeneza pasi nyingi ambazo ni 13 za mabao. Pasi yake ya kwanza alitoa kwenye mchezo dhidi ya KMC FC alimpa mshikaji wake Idd Nado.
Ni mabao manne alifunga msimu wa 2024/25 hivyo kahusika kwenye mabao 17 kati ya 56 yaliyofungwa na timu hiyo iliyomaliza ligi ikiwa nafasi ya tatu na pointi 63. Baada ya kucheza mechi 30 ambazo ni dakika 2,700 alianza kikosi cha kwanza mechi 26.
Hivi karibuni, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Azam FC, Thabit Zakaria aliweka wazi kuwa Feisal atakuwa ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2025/26.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.