THANK YOU SIMBA SC ZIMEPITA KWA MIAMBA HAWA MAZIMA

THANK You ndani ya kikosi cha Simba SC zinaendelea ambapo kuna mastaa ambao wamekutana nazo na wengine walianza wao kutoa hivyo hawatakuwa ndani ya timu hiyo kwa msimu wa 2025/26.

Ni Fabrince Ngoma kiungo wa kazi alikuwa wa kwanza kutoa Thank You ambapo alibainisha kuwa walifanya kazi kwa ushirikiano ndani ya kikosi hicho licha ya kushindwa kutwaa mataji.

Valentino Nouma ingizo jipya kwa msimu wa 2024/25 naye pia hatakuwa ndani ya kikosi cha Simba SC msimu ujao baada ya kupewa Thank You.

Nouma alipewa Thank You Julai 12 2025. Kwa sasa ni mchezaji huru atajiunga bure na timu ambayo itafikia makubaliano.

Beki Hussen Kazi ambaye hakucheza mchezo hata mmoja kwa msimu wa 2024/25 naye ameondoka. Beki Hussen Kazi alipewa Thank You rasmi na Simba SC Julai 13.

Agustine Okejapha alipewa Thank You rasmi na Simba SC Julai 13 2025. Mbali na hawa kipa Aishi Manula ambaye aliibuka ndani ya Simba SC akitokea Azam FC, amrejea kwa mara nyingine Azam FC na sasa atakuwa kwenye changamoto mpya.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.