KIUNGO wa Yanga SC Pacome Zouzoua ambaye mkononi ana tuzo ya mchezaji bora ndani ya Ligi Kuu Bara inayodhaminiwa na NBC msimu wa 2024/25 ndani ya Juni 2025 anatajwa kuwa atasalia ndani ya kikosi hicho kwa msimu ujao wa 2025/25.
Pacome alikuwa kwenye mwendo bora ndani ya uwanja msimu uliopita akiwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ambaye naye alitwaa tuzo ya kocha bora ndani ya Juni. Ipo wazi kwamba msimu wa 2025/26 Yanga SC itakuwa na kocha mpya baada ya Miloud kuondoka.
Tayari kocha mpya wa Yanga SC ameshatua ndani ya Dar muda wowote kuanzia sasa atatambulishwa. Taarifa zinaeleza kuwa kocha mpya ni raia wa Ufaransa anaitwa Julien Chavelier aliyekuwa anaifundisha Asec Mimosas ya nchini Ivory Coast.
Pacome inaelezwa kuwa ameongezewa kandarasi ya miaka miwili kuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC kilichotwaa ubingwa wa ligi baada ya mechi 30 ambazo ni dakika 2,700. Pointi kibindoni ni 82 na safu ya ushambuliaji ilifunga mabao 82.
Pacome ni mabao 12 alifunga na kutoa pasi 10. Alihusika kwenye mabao 22 kati ya 83. Bao lake la 12 alifunga kwenye mchezo dhidi ya Simba SC ilikuwa Juni 25 2025 na alitoa pasi ya 10 kwenye mchezo huo alimpa Clement Mzize ambaye amefikisha jumla ya mabao 14 ndani ya ligi.
Rekodi zinaonyesha kuwa ni mechi 26 alicheza za ligi akikomba dakika 1,614. Mguu wake wenye nguvu ni ule wa kulia ambao umefunga mabao 7 huku ule mguu wa kushoto ukifunga mabao manne na bao moja alifunga kwa pigo la kichwa. Ni mtoa pasi wa kwanza wa bao ndani ya Yanga SC ilikuwa dakika ya 25 alimpa Maxi Nzengeli dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.