Kuna siku ambazo hazifutiki katika kalenda ya soka, na Julai 13, 2025, ni mojawapo. Uwanja wa MetLife, New Jersey, umegeuka jukwaa la kihistoria. Chelsea, timu iliyopuuzwa na wengi mwanzoni mwa mashindano, wameandika upya ramani ya dunia kwa kushinda Kombe la Dunia la Klabu kwa mara ya pili. Lakini hadithi hii haikuanza kwenye fainali, ilianza kimya kimya, miezi kadhaa nyuma, wakati ambapo matumaini yalikuwa madogo, lakini ndoto zilikuwa kubwa.
Mashindano haya ya kihistoria, yakiwa ya kwanza kwa mfumo wa vilabu 32, yalizinduliwa kwa shamrashamra kubwa Marekani. Viwanja vya kisasa vilijaa, nyimbo zikaimbwa, na dunia ilishikilia pumzi kusubiri majibu, nani angetwaa taji la dunia kwa vilabu?
Chelsea waliingia kundi D wakiwa hawana presha. Walikuwa miongoni mwa vilabu vya Ulaya vilivyofuzu kwa rekodi ya miaka minne iliyopita. Wakipangwa na mabingwa wa Afrika, Asia na Amerika Kusini, walipambana kwa nidhamu ya jeshi na wakamaliza kundi lao wakiwa kinara. Kule kundi B, PSG walitamba, wakiongozwa na mastaa kama Dembele, Hakimi, na Fabian Ruiz. Bayern Munich, Palmeiras, Real Madrid, Juventus na Inter Miami wote waliendelea, kila mmoja akiwa na matumaini ya kulitwaa kombe hilo.
NB: Jisajili na Meridianbet na cheza michezo ya kasino ya mtandaoni upate ushindi kirahisi, Pia ongeza maokoto yako kwa kubashiri michezo mbalimbali yenye ODDS KUBWA. PIGA *149*10# AU tembelea tovuti yao meridianbet.co.tz
Uwanja wa MetLife ulijaa hadi kufurika ilipofika tarehe 13, tarehe iliyongojewa na wengi. PSG walikuja na kila silaha, kasi ya Dembele, uzoefu wa Fabian, na maelekezo ya kocha mkongwe Luis Enrique. Lakini Chelsea walikuwa tayari kimwili na kiakili. Dakika 90 za mchezo ziligeuka maonyesho ya soka safi. Cole Palmer, kijana aliyetokea kwenye akademi ya Manchester City, aliwazima PSG kwa mabao mawili na kutoa pasi ya bao la tatu. Chelsea 3, PSG 0.
Hawakushinda kwa bahati. Walishinda kwa sababu walielewana kama familia, waliheshimu kila dakika ya mchezo, na walicheza bila hofu. Baada ya kipenga cha mwisho, wachezaji wa Chelsea walilia si kwa huzuni, bali kwa furaha ya safari ya mapambano waliyoimaliza kwa kishindo.
Kwa upande wa mashabiki, hasa waliokuwa na Meridianbet, furaha hiyo ilikuwa maradufu. Odds ya ushindi wa Chelsea ilikuwa 5.40 dhidi ya 1.63 ya PSG. Waliowaamini Chelsea walizawadiwa vizuri. Waliopiga multi-bet kwenye hatua za nyuma walicheka na benki. Meridianbet iliwapa fursa ya kuwa sehemu ya historia kwa kila mechi, kila bao, na kila tukio.
Sasa Chelsea wameandika historia mpya. Si mabingwa wa England tu, si wa Ulaya tu bali wamevikwa taji la dunia. Ni hadithi ya soka safi, ya kupigana, ya kutokuogopa majina makubwa. Na kwa mashabiki walioweka imani yao kupitia Meridianbet, huu haukuwa ushindi wa Chelsea pekee ulikuwa ushindi wao pia.