MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, inayodhaminiwa na NBC Yanga SC msimu wa 2024/25 wapo kwenye hesabu kupitisha panga la moto. Timu hiyo ilitwaa ubingwa ikiwa na pointi 82 na safu ya ushambuliaji ilifunga mabao 83.
Miloud Hamdi ameshasepa ndani ya Yanga SC alitangazwa kuwa kocha bora ndani ya Juni 2025 na mchezaji bora ni Pacome kwenye ligi. Miloud akiwa ameshasepa tayari mrithi wake yupo Dar akiwa kwenye uangalizi mkubwa kutazama ripoti ambapo kuna panga litapitishwa hivi karibuni.
Wakati panga hilo likitajwa kumpitia Clatous Chama, Jonas Mkude, Dennis Nkane kuna majina ambayo yanatajwa kwa karibu ni staa wa Ivory Coast, Mohamed Doumbia na Celestin Ecua.
Doumbia tayari yuko Tanzania na alionekana akifuatilia mechi ya Ligi Kuu ya NBC kati ya Yanga na Dodoma ambayo ilifanyika visiwani Zanzibar. Ukiachana na Doumbia, macho ya uongozi wa Yanga pia yanafuatilia kwa karibu nyota, Célestin Ecua ambaye msimu uliopita Ecua alifunga goli 15 na assists 12.
Pacome Zouzoua na Maxi Nzengeli inaelezwa kuwa wapo kwenye mchakato wa kusaini mikataba mipya kuendelea kusalia ndani ya timu hiyo.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.