TANZANIA INAHESABU ZA UBINGWA WA CHAN

KUELEKA CHAN 2024, wachezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars wapo nchini Misri kwa kambi maalumu huku hesabu kubwa ikiwa ni kupata matokeo kwenye mechi zijazo za ushindani na kutwaa ubingwa kwa kupata matokeo chanya katika uwanja.

Dickson Job ambaye ni beki mwenye uwezo wa kupiga pasi ndefu na fupi ni miongoni mwa wachezaji waliopo Misri, amesema kuwa wanafanya maandalizi mazuri ambayo yatawapa matokeo mazuri huku hesabu ikiwa ni kutwaa ubingwa katika mashindano hayo makubwa.

“Tumejiandaa na tupo tayari kwa mashindano ambayo yapo mbele yetu. Maandalizi ambayo tunayafanya ni imara na wachezaji tupo tayari kufanya vizuri. Nina amini kwa ushirikiano na matumaini yetu ni kuona kwamba tunatwaa ubingwa.

“Ninachoamini kwamba mashindano haya ni makubwa na tunatamani kunafanya makubwa. Nikiwa mchezaji ninafurahi kuwa katika maandalizi haya. Ninapenda kufanya vizuri na tunatamani kufanya vizuri kwa kuwa ni wakati wangu kujitangaza kwenye mashindano haya makubwa.

“Makubwa ni kitu ambacho tunapenda kufanya na hasa kufanya vema kwenye mashindano haya yenye ushindani natamani kufanya makubwa na timu yangu ya taifa hivyo tukifanya maandalizi yaliyo bora na kufanya vema tutakwenda kuchukua ubingwa,” amesema Job.

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ipo kwenye maandalizi kuelekea CHAN 2024 ambapo mazoezi wanafanyia katika Viwanja vya Mercure, Misri.

Agosti 2 2025 Uwanja wa Mkapa zikiwa zimesalia siku 20 utachezwa mchezo wa ufunguzi kati ya Tanzania na Burkina Faso ambapo Tanzania, Kenya, Uganda ni wenyeji wa mashindano huku Tanzania ikichaguliwa kucheza mchezo wa ufunguzi.

Tanzania ipo Kundi B lenye timu za Tanzania, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Central Africa Republic.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.