KIUNGO wa Yanga Pacome Zouzoua amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Juni wa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2024/2025, akiwashinda Clatous Chama wa Yanga na Kibu Denis wa Simba, alioingia nao fainali katika mchakato wa Tuzo za Mwezi uliofanywa na Kamati ya Tuzo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Pacome raia wa Ivory Coast alionesha kiwango kizuri chenye mwendelezo akitoa mchango mkubwa kwa timu yake katika michezo mitatu ambayo Yanga ilicheza mwezi huo ambapo alifunga mabao matatu na kuhusika na bao moja kwa dakika 242 alizocheza.