Dar es Salaam, Tanzania – Klabu ya Yanga SC kupitia kwa Msemaji wake, Alikamwe, leo imezindua rasmi kampeni mpya iitwayo “Tofali la Ubingwa” inayolenga kuchangisha fedha kutoka kwa mashabiki na wanachama ili kusaidia timu katika usajili wa wachezaji wenye ubora wa hali ya juu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Kamwe amesema kampeni hii ni sehemu ya mkakati wa klabu kujitegemea na kuwa na nguvu ya kiuchumi inayotokana na mashabiki wake, ambao wamekuwa mstari wa mbele kuiunga mkono timu katika mafanikio yake.
“Kampeni hii itaiwezesha Yanga kusajili wachezaji bora kwa kutumia fedha zitakazotokana na michango ya mashabiki. Tunataka kila mshabiki ajihusishe moja kwa moja na mafanikio ya timu kwa kuweka tofali lake kwenye msingi wa ubingwa wa Yanga,” alisema Kamwe.