KIUNGO wa kazi ndani ya Yanga SC, Clatous Chama yupo kwenye hesabu za mwisho kujiunga na Klabu ya Zesco United ambayo nahitaji huduma yake.
Julai Mosi 2024, Chama alitambulishwa ndani ya kikosi cha Yanga SC kwa kandarasi ya mwaka mmoja ambayo imegota mwisho.
Inaelezwa kuwa alikuwa kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba wake ila kuna vipengele ambavyo ilikuwa ni ngumu kufikia jambo ambalo limefanya awe kwenye asilimia kubwa kutokuwa ndani ya kikosi cha Yanga SC.
Ikumbukwe kwamba msimu wa 2024/25 Chama hakuwa chaguo la kwanza kwa makocha wote watatu ambao walikuwa wakiifundisha Yanga SC.
Ni mabao 6 alifunga na kutoa pasi tatu za mabao ndani ya ligi. Alihusika kwenye mabao 9 kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga SC.
Yanga SC ni mabingwa wa msimu wa 2024/25. Ni pointi 82 walikomba baada ya mechi 30 ambazo ni dakika 2,700.
Tayari dirisha la usajili limefunguliwa ilikuwa Julai Mosi 2025 linatarajiwa kufungwa Septemba 7 2025.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.