Klabu ya RS Berkane kutoka Morocco wamefungua rasmi mazungumzo ya awali na upande wa mchezaji Elie Mpanzu, ambaye kwa sasa ni nyota wa Simba SC.
Hawajatuma ofa rasmi kwa Simba SC bado, bali wanataka kwanza kukubaliana na mchezaji kuhusu maslahi binafsi kama mshahara na bonasi.
Vyanzo vinaeleza kuwa RS Berkane wako tayari kulipa kifungu cha kuvunja mkataba (release clause) ambacho Simba waliweka kwa mchezaji huyo – kikadiriwa kuwa ni takriban Tsh milioni 450.
RS BERKANE WAANZA MAZUNGUMZO NA KAMBI YA ELIE MPANZU
