CHAMA CLATOUS ATAJWA KUONDOKA YANGA SC

INAELEZWA kuwa kiungo mshambuliaji wa Yanga SC ambaye aliibuka hapo akitokea Simba SC, Clatous Chama huenda akaondoka ndani ya timu hiyo baada ya mkataba wake kugota mwisho.

Mbali na Chama kusepa Yanga SC taarifa za kuaminika kutoka ndani ya Yanga SC zimethibitisha kuwa, timu hiyo imefikia makubaliano ya kuachana na mastaa wao wengine wa ushambuliaji ambao ni kiungo Mkongomani, Jonathan Ikangalombo na straika Mzambia Kennedy Musonda.

Musonda na Yanga wameachana Rasmi. Mkataba wa Musonda mwenye umri wa miaka 30 na Yanga SC umeisha na mchezaji huyo ameondoka jangwani kwa ajili ya kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine.

Musonda atakumbukwa na wananchi kwa mchango wake mkubwa, ikiwemo bao moja alilofunga katika ushindi wa kihistoria wa mabao 5-1 dhidi ya Simba SC msimu  wa 2023/24. Mchezo huo ulipigwa kwenye Uwanja wa Benjamina Mkapa Dar es Salaam.

Msimu wa 2024/25 Musonda amegotea kufunga mabao matatu ndani ya Yanga SC ambayo imemaliza msimu ikiwa namba moja kwa kufunga mabao mengi ambayo ni 83 na pointi zake kibindoni ni 82 baada ya mechi 30.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.