MATAJIRI wa Dar, Azam FC hawapoi baada ya kumtambulisha nyota mwingine mpya ambaye aliwahi kucheza hapo kabla ya kuondoka kuelekea Misri kwa changamoto mpya.
Kazi imeanza kwa timu hiyo ambayo itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa imegotea nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi msimu wa 2024/25.
Ni Kocha Mkuu, Florent Ibenge atakuwa kwenye benchi la ufundi la timu hiyo ambayo inatumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi za nyumbani.
Nyota mwingine ambaye amerejea ni Himid Mao kiungo wa kazi ngumu amerejea ndani ya kikosi cha Azam FC na kupewa kandarasi ya mwaka mmoja itakayodumu mpaka 2026 akiwa kwenye kikosi hicho.
Mbali na Himid nyota mwingine ambaye amerejeshwa katika kikosi hicho ni Aishi Manula ambaye alikuwa ndani ya kikosi cha Simba SC anarejea kwa ajili ya kuendelea na majukumu yake kuelekea msimu wa 2025/26.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.