MPANZU WA SIMBA SC KWENYE RADA ZA WAARABU

INAELEZWA kuwa winga chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids ndani ya kikosi cha Simba SC, Ellie Mpanzu yupo kwenye rada za RS Berkane,Waarabu wa Morocco.

Mpanzu ni miongoni mwa wachezaji waliokuwa tegemeo katika kikosi cha Simba SC msimu wa 2024/25 kwenye anga la kimataifa na kitaifa.

Ndani ya ligi rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 17 kati ya 30. Ikumbukwe kwamba Mpanzu aliibuka ndani ya Simba SC kwenye dirisha dogo la usajili.

Simba SC ikiwa imefunga mabao 69 kahusika kwenye mabao 7, akifunga manne na kutoa pasi tatu. Ni dakika 1,239 alikomba uwanjani.

Ikiwa RS Berkane wataipata saini yake, Simba SC itakuwa na kazi kusaka winga mwingine ambaye atakuja katika kikosi hicho.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.