HILI HAPA JAMBO KUBWA LINAFUATA KWA AZAM FC

MATAJIRI wa Dar Azam FC wanakuja na jambo kubwa jingine ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu wa 2025/26 unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Azam FC imekamilisha mzunguko wa pili msimu wa 2024/25 ikiwa na pointi 63 itashikriki Kombe la Shirikisho Afrika tayari imeanza kutambulisha wachezaji wake wapya.

Julai 3 2025 ilimtambulisha beki mzawa kutoka Coastal Union, Lameck Lawi ambaye amejifunga miaka miwili atakuwa hapo mpaka 2027.

Ni uzi mpya ni jambo kubwa jingine ambalo linafuata kwa Azam FC inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwenye mechi zake za nyumbani.

Julai 6 2025 uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika ambapo itakuwa ndani ya viwanja vya Sabasaba, Dar, saa 5:00 asubuhi.

Mzigo tayari umeshafika ambapo tambo za Azam FC wao wanasema, “Raundi hii mtavurugwa sana.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.