ISRAEL Mwenda, beki wa kulia wa Yanga SC ndani ya kikosi cha Yanga SC alikimbiza kwa muda mfupi ambao alitua hapo.
Mwenda alikuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi na kwenye mchezo dhidi ya mabosi wake wa zamani Simba SC alipewa kazi maalumu kumkaba Ellie Mpanzu nyota wa Simba SC.
Mwenda ameweka wazi kuwa ni furaha kubwa kwa Yanga SC kupata matokeo na kuwa mabingwa jambo ambalo linawafanya waendelee kufikiria kuwa bora zaidi msimu ujao.
“Ulikuwa ni msimu wenye mafanikio na furaha kwetu.Wengine ninawaambia kwamba watoroke waje Yanga SC huku kuna makombe na kazi inaendelea.”
Mwenda alisajiliwa na Yanga SC akitokea Singida Black Stars. Ndani ya Yanga SC msimu wa 2024/25 ni mechi 13 alifunga mabao matatu na pasi mbili kati ya mabao 83 yaliyofungwa na Yanga SC.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.