KOCHA WA AL HILAL KUINOA AZAM FC MSIMU MPYA?

KOCHA Mkuu wa Al Hilal Omdurman ya nchini Sudan, Florent Ibenge inatajwa kuwa amemalizana na matajiri wa Dar, Azam FC kuwa kwenye benchi la ufundi kwa msimu wa 2025/26.

Inaelezwa kuwa Ibenge amemalizana na Azam FC kwa ajili ya msimu ujao unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Azam FC msimu wa 2024/25 imeambulia patupu kwenye mataji ikiwa imegotea nafasi ya pili kwenye msimamo na pointi 63 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 56.

Kuna uwezekano mkubwa kocha huyo akawa kwenye ardhi ya Tanzania akitimiza majukumu yake ndani ya Azam FC inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwa mechi za nyumbani.
Akizungumza na Global Publisher, Mkuu wa Idara ya Habari ndani ya Azam FC, Zakaria Thabit maarufu kama Zakazakazi kuhusu ujio wa Ibenge alibainisha kuwa naye anaskia taarifa hizo.
“Hata mimi ninaskia kuhusu taarifa hizo ambazo unauliza. Kwa hiyo kama kutakuwa na taarifa yoyote kwenye upande wa michezo hilo litakuwa wazi na litafahamika hakuna kitakachofichwa.”