NYOTA wawili kutoka Azam FC ambao wanatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Yanga SC wametajwa na bosi wa kutoka mitaa ya Jangwani.
Ni Feisal Salum kiungo mshambuliaji ambaye ni kinara kwa utengenezaji pasi za mwisho akiwa nazo 13 na Giblil Sillah mwenye pasi mbili za mabao.
Mbali na pasi mbili za mabao alizonazo Sillah kiungo huyo mshambuliaji katupia jumla ya mabao 9 kwenye ligi huku Feisal akiwa katupia mabao manne.
Mastaa hawa wanatajwa kuwa kwenye rada za timu mbalimbali na miongoni mwa timu ambazo zinatajwa ni Yanga SC.
Kuhusu Fei mabosi wa Azam FC waliweka wazi kuwa bado mchezaji huyo yupo ndani ya kikosi hicho kwa kuwa walisubiri ofa na hakuna timu iliyofika hapo.
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa kwa timu kuwa na wachezaji wazuri ni sababu kutokuwa na hofu kuona watu wanaangalia mchezo.
“Ikiwa unakuwa na wachezaji wazuri kama Pacome, una Sillah una mchezaji kama Feisal unadhani utakuwa na hofu kuona kuna watu wanakuja kuiangalia timu yako? Huwezi kuwa na hofu kwa kuwa una wachezaji wazuri wenye uwezo.”
Sillah kwenye mabao 9 aliyofunga kazifunga Simba SC na Yanga SC kwenye ligi bao mojamoja walipokutana.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.