SIMBA SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids, kesho Mei 31 2025 watakuwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa kwenye msako wa ushindi.
Ni mchezo wa hatua ya nusu fainali CRDB Federation Cup inawakutanisha wababe hao waliotoka kuvaana kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa KMC Complex.
Katika mchezo huo uliochezwa Mei 28 2025 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 1-0 Singida Black Stars.
Bao la ushindi kwenye mchezo lilifungwa na Steven Mukwala dakika ya 42 akitumia pasi ya Jean Ahoua. Mukwala na Shomari Kapombe ni miongoni mwa wachezaji waliokutwa kwenye mtego wa kuotea mzunguko wa pili.
Mshindi wa mchezo wa Mei 31 2025 atatakata tiketi kucheza fainali na Yanga SC iliyopata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Tanzania.
Mohamed Hussein Zimbwe Jr nahodha wa Simba SC ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wa nusu fainali na wanatambua ugumu uliopo kwa wapinzani wao.
“Tunajua ni mchezo mgumu ambao ni hatua ya nusu fainali, ambacho tunahitaji ni kupata matokeo mazuri uwanjani mashabiki wajitokeze kwa wingi.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.