Lamine Yamal amesaini mkataba utakaomuwezesha kuendelea kubakia na FC Barcelona hadi mwaka 2030, klabu hiyo ilitangaza Jumanne ,
Maelezo ya mkataba huo – ambao ulitiwa saini katika ofisi za klabu mbele ya rais Joan Laporta na mkurugenzi wa michezo Deco – hayakutolewa na Barca, lakini ripoti nyingi kutoka kwa vyombo vya habari vya Uhispania zinasema kwamba kijana huyo nyota wa soka mwenye umri wa miaka 17, anatarajiwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi kwenye kikosi na uwezekano wa mshahara wa kila mwaka wa takriban euro milioni 19 (kama dola milioni 21) baada ya kukatwa ushuru.