MSHAMBULIAJI wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi anatajwa kuwa kwenye rada za mabosi wa Misri ambao wanahitaji saini yake.
Mzize ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud kafunga mabao 13 msimu wa 2024/25 akiwa ni mzawa namba moja kwa washambuliaji wenye mabao mengi.
Taarifa zinaeleza kuwa Klabu ya Zamalek imewasiliana na Yanga SC ili kuipata saini ya mshambuliaji Clement Mzize.
Nyota Mzize mwenye miaka 21 inaelezwa kuwa kwa sasa mazungumzo yameanza na hadi sasa yamefikia pazuri katika kumpata nyota huyo.
Zamalek SC wanapambana kukamilisha dili hilo kwa wakati, na huo unatarajiwa kuwa usajili wa kwanza kuelekea msimu ujao katika kikosi hicho.
Mzize huenda akawa mchezaji wa pili kununuliwa katika kikosi cha Yanga, baada ya kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki kununuliwa Wydad Athletic ya Morocco.
Tayari Aziz Ki ameshatambulishwa kwenye timu yake mpya ilikuwa Mei 25 2025 kwa ajili ya changamoto mpya kwa msimu wa 2025/26.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.