SELEMAN Matola, kocha msaidizi wa Simba SC amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wao ujao wa ligi dhidi ya Singida Black Stars ambao ni mzunguko wa pili.
Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Liti baada ya dakika 90 ubao ulisoma Singida Black Stars 0-1 Simba SC.
Bao la ushindi kwenye mchezo huo lilifungwa na Fabrince Ngoma kwa pasi ya Jean Ahoua ambaye alipiga kona ya moja kwa moja iliyokutana na kichwa cha Ngoma.
Matola amesema kuwa wapinzani wao wapo imara kutokana na aina ya timu waliyonayo pamoja na kikosi bora walichonacho.
“Tunakwenda kukutana na timu ngumu ambayo ina kikosi imara hilo tunajua lakini ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu, tupo tayari na mchezo hautakuwa mwepesi.”
Simba SC kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi69 inakutana na Singida Black Stars iliyo nafasi ya nne na pointi 53.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.