SIMBA SC VS RS BERKANE MEI 25 2025, KIKOSI HIKI HAPA

SIMBA SC chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids ina kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya RS Berkane mchezo wa fainali ya pili Kombe la Shirikisho Afrika, Mei 25 2025, Uwanja wa New Amaan Complex.

Mchezo wa kwanza Simba SC ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 hivyo kazi yao kwenye kutwaa ubingwa ambao RS Berkane wanahitaji ni kupata mabao 3-0 ndani ya dakika 90.

Hiki hapa kikosi cha Simba SC ambacho kinatarajiwa kuanza kipo namna hii:-

Moussa Camara ameanza langoni ukiwa ni mchezo wake wa pili kwenye fainali zote ile ya ugenini na leo wakiwa nyumbani.

Chamou, Fabrince Ngoma, Jean Ahoua, Steven Mukwala, Shomari Kapombe, Mohamed Hussen ambaye ni nahodha, Che Malone, Yusuph Kagoma, Joshua Mutale, Ellie Mpanzu ambapo Kibu Dennis aliyeanza mchezo uliopita akikomba dakika 45 ameanza benchi.

Wachezaji wengine wa akiba ni Salim Ally, Duchu, Nouma, Okejapha, Chasambi, Mavambo, Leonel Ateba, Awesu Awesu.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.