LIVE: SIMBA SC 1-1 RS BERKANE, FAINALI, MEI 25 2025

FT: Uwanja wa New Amaan Complex

Simba SC 1-1 RS Berkane, (1-3)

RS Berkane wanapata bao la kuweka usawa dakika ya 90.

Dakika ya 70 Steven Mukwala alipachika bao ambalo VAR limefuta kwa kueleza kuwa alikuwa kwenye mtego wa kuotea.

Yusuph Kagoma kiungo wa Simba SC ameonyeshwa kadi mbili za njano na kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 50.

Mapumziko.

Simba SC 1-1 RS Berkane, (Agregate 1-3)

Dakika ya 41 Joshua Mutale anachezewa faulo na Ayoub wa RS Berkane ambaye anaonyeshwa kadi ya njano.

Fadlu Davids Kocha Mkuu wa Simba SC na Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba SC, Shomari Kapombe beki wa Simba SC wameonyeshwa kadi kila mmoja ya njano dakika ya 35.

Dakika ya 30 Jean Ahoua anaipiga kona ya pili kwa Simba SC.

Dakika ya 22 Shomari Kapombe jaribio lake akiwa ndani ya 18 linakwenda nje ya lango.

Joshua Mutale anafunga bao kwa Simba SC dakika ya 15 kwa mguu wa kushoto akimalizia pasi ya Ellie Mpanzu.

Dakika 1o Joshua Mutale anapiga pasi ndefu kuelekea lango la RS Berkane inadakwa na kipa

Dakika ya 9 Yusuph Kagoma alicheza faulo kwa mchezaji wa RS Berkane

Fainali ya pili Kombe la Shirikisho Afrika.

SIMBA SC ya Tanzania ina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya RS Berkane kwenye mchezo wa fainali Mei 25 2025, kwenye mchezo wa kwanza Mei 17 ubao ulisoma RS Berkane 2-0 Simba SC.

Simba SC ina kazi kusaka ushindi wa mabao 3-0 ili kutwaa taji hilo ambalo lipo kwenye ardhi ya Tanzania.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.