WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa Simba SC chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids hesabu kubwa ni kuingia kwa mkakati kuwakabili wapinzani wao RS Berkane kwenye mchezo wa fainali ya pili Kombe la Shirikisho Afrika.
Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba SC ameweka wazi kuwa wanatambua mchezo uliopita walipoteza ila mchezo wa pili kwa kuwa watakuwa nyumbani kazi kubwa itafanyika kupata matokeo.
Ugenini Mei 17 2025 baada ya dakika 90 ubao ulisoma RS Berkane 2-0 Simba SC, mchezo wa pili utaamua nani atatwaa taji hilo utapigwa Mei 25, Jumapili kwenye ardhi ya Tanzania, Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.
RS Berkane walianza kupata mabao ndani ya dakika 15 za mwanzo yalidumu mpaka mwisho wa mchezo huo wa kwanza ilikuwa kupitia kwa Mamadou Camara dakika ya 8 na Ousama Lamlioui dakika ya 15 waliomtungua Mousa Camara kipa namba moja wa Simba SC.
Fadlu amesema: “Kazi ni kubwa baada ya kupoteza mchezo wetu wa kwanza tuliangalia makosa, wachezaji walifanya kazi kubwa hivyo kwenye mchezo wetu wa pili tunapaswa kujitoa zaidi ili kupata matokeo mazuri.”
Simba SC ili kutwaa taji la Kombe la Shirikisho Afrika ni lazima ipate ushindi wa mabao 3-0 kwenye mchezo wa pili wakiwa nyumbani.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.