AZIZ KI REKODI ZAKE BONGO BALAA

AZIZ Ki kiungo mshambuliaji wa Yanga SC rekodi zake ndani ya timu hiyo ni balaa kutokana na kuwa miongoni mwa nyota waliotoa pasi nyingi za mabao kwenye mechi za ushindani akiwa na jezi namba 10.

Ki ndani ya kikosi cha Yanga SC rekodi zinaonyesha kuwa ni mechi 114 alicheza akitoa jumla ya pasi 57 na kufunga jumla ya mabao 32.

Bao lake la kwanza kufunga ndani ya ligi ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo alianzia benchi katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa na alimtungua kipa Faroukh Shikalo.

Ilikuwa ni Septemba 13,2022 Uwanja wa Mkapa dakika ya 90 alipachika bao lake la kwanza akitokea benchi na alimtungua Faroukh Shikalo aliyekuwa langoni akiwa nje ya 18 kwa mguu wa kushoto jambo lililompa lawama kipa huyo.

Nyota huyo msimu wake wa kwanza akiwa na uzi wa Yanga SC alitupia mabao 9 kibindoni na alitoa jumla ya pasi tano za mabao baada ya kucheza jumla ya mechi 23 ndani ya msimu wa 2022/23.

Katika msimu wake wa kwanza ndani ya Yanga SC alihusika kwenye mabao 14 kati ya 56 ambayo yalifungwa na timu hiyo iliyotwaa ubingwa wa ligi ikiwa na pointi 74.

Kwa msimu wa 2024/25 mchezo wake wa mwisho ulikuwa dhidi ya JKT Tanzania alianza kikosi cha kwanza kwenye hatua ya nusu fainali na mwisho ubao wa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga ulisoma Yanga SC 2-0 JKT Tanzania.

Yanga inatinga hatua ya fainali CRDB Federation Cup itakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba SC vs Singida Black Stars unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Tanzanite Kwaraa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.