HII HAPA ORODHA YA WAKALI WA KUCHEKA NYAVU

WACHEZAJI ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora wanapambana katika kutimiza majukumu yao ndani ya uwanja msimu wa 2024/25.

Kwenye eneo la ufungaji kuna wakali katika kucheka na nyavu hapa tunakuletea orodha yao namna hii:-

Jean Ahoua-15

Jean Ahoua  kiungo mshambuliaji wa Simba SC yeye ni namba moja akiwa katupia mabao 15.

Mzize-13

Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga SC anaingia kwenye orodha ya wakali katika kucheka na nyavu akiwa ametupia mabao 13 yupo kikosi cha Yanga SC.

Dube-13
Prince Dube nyota ambaye anaingia kwenye rekodi ya kuwa wa kwanza kufunga hat trick aliyofunga dhidi ya Mashujaa anaingia kwenye orodha ya wakali wa kucheka na nyavu akiwa katupia mabao 13.

Lionel Ateba -12

Leonel Ateba mshambuliaji wa Simba SC yeye kibindoni ametupia jumla ya mabao 12.

Steven Mukwala- 11

Steven Mukwala mshambuliaji mrefu kuliko goli yupo ndani ya kikosi cha Simba SC akiwa katupia jumla ya mabao 11.

Jonathan Sowah-11

Jonathan Sowah kasi yeke ni nzito yupo ndani ya kikosi cha Singida Black Stars akiwa katupia mabao 11.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.