INAELEZWA kuwa kiungo wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga SC kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi, Aziz Ki anasepa mazima ndani ya kikosi hicho baada ya kupata ofa kutoka Wydad ambayo inahitaji huduma yake.
Taarifa zinaeleza kuwa kuna uwezekano mkubwa kiungo huyo akaondoka mapema kujiunga na timu mpya kwa ajili ya changamoto mpya.
Ki ambaye ni mchezaji bora msimu wa 2023/24 alikuwa anatajwa kuwa miongoni mwa nyota ambao watasepa ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika msimu utakapogota mwisho kutokana na ofa ambazo zipo mezani.
Mbali na Wydad ambao wanapewa chapuo kubwa kuinasa saini yake inaelezwa kuwa Kaizer Chiefs nao wanahitaji huduma ya kiungo huyo mwenye uwezo wa kutumia mguu wa kushoto.
Tetesi zinaeleza kuwa Aziz huenda akapewa mkono wa asante ndani ya Yanga SC kutokana na dau kubwa ambalo limewekwa na timu ambazo zinamuhitaji.
Kiungo huyo alianza kikosi cha kwanza kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga hatua ya nusu fainali CRDB Federation Cup na Yanga SC wakikata tiketi ya kutinga hatua ya fainali wakimsubiri mshindi kati ya Simba SC ama Singida Black Stars kwenye mchezo wao unaotarajiwa kuchezwa Mei 31 2025.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.