YANGA SC KAMILI KUIKABILI JKT TANZANIA MEI 18 2025

  • Khalid Aucho amerejea uwanja wa mazoezi kamili kwa kazi kuwakabili JKT Tanzania.

  • Yanga SC ni mabingwa watetezi wa taji hilo

  • Pacome kiungo wa kazi anatarajiwa kuwa miongoni mwa watakaotoa burudani, Mkwakwani Tanga

YANGA SC chini ya Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ipo kamili kuwakabili wapinzani wake kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya JKT Tanzania unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Ikumbukwe kwamba Yanga SC ni mabingwa watetezi wa taji hilo walitwaa mbele ya Azam FC ambayo kwa msimu wa 2024/25 ilifungashiwa virago na Mbeya City, Uwanja wa Azam Complex.

Mapema Mei 16 msafara wa Yanga SC uliwasili Tanga kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuwakabili JKT Tanzania na miongoni mwa wachezaji waliopo ni Khalid Aucho, Pacome, Dickson Job, Jonas Mkude.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wao dhidi ya JKT Tanzania na mpango mkubwa ni kuona wanapata matokeo mazuri ili kusonga mbele.

“Mchezo wetu dhidi ya JKT Tanzania tupo tayari kwa mapambano ni mchezo utakaokuwa na ushindani mkubwa. Baada ya matokeo mazuri tunaamini tutakuwa na mchezo mwingine wa hatua ya fainali hivyo mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.”

Mshindi wa mchezo wa Mei 18 2025 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Singida Black Stars unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.