ROBERTINHO AWASILISHA MALALAMIKO FERWAFA AKIDAI DOLA 20,000

Kocha Robertinho ambaye hivi majuzi alisimamishwa na Rayon Sports kwa sababu za kimatibabu, amewasilisha malalamiko kwa Chama cha soka cha Rwanda (FERWAFA) akitaka kulipwa Dola za Kimarekani 20,000 Mshahara wa miezi minne.

Kocha huyo tayari ameiandikia barua FERWAFA akiomba kulipwa mishahara ya miezi minne sawa na Dola 20,000 na ndani ya wiki tatu kabla ya kupeleka mashitaka yake shirikisho la soka Duniani (FIFA).

Robertinho (64), ambaye analipwa Dola 5,000 kwa mwezi, hivi majuzi aliiomba Rayon Sports kumlipa deni lake na kurejea nyumbani kwao Brazil kwa sababu hana la kufanya Kigali.

Kocha huyo alikuwa amesimamishwa siku 30 na Rayon Sports ikiwa na maana kuwa msimu kwake ulikuwa umemalizika.