YANGA SC YAVUNA SITA POINTI MBELE YA NAMUNGO

YANGA SC imevuna pointi sita mbele ya wapinzani wao Namungo FC kwa kupata ushindi kwenye mechi zote mbili ambazo walikutana ndani ya uwanja katika dakika 180 za kusaka pointi.

Ikumbukwe kwamba Mei 13 2025 ulikuwa ni mchezo wa mzunguko wa pili baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Yanga SC 3-0 Namungo FC.

Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Novemba 30 2024 ubao wa Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 0-2 Yanga, mabao ya Kennedy Musonda na Pacome yalitosha kuipa Yanga SC pointi tatu.

Mei 13 2025 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Yanga SC 3-0 Namungo FC. Kwenye msako wa pointi sita ndani ya msimu wa 2024/25 Yanga SC kakomba zote na safu ya ushambuliaji imetupia mabao matano.

Djigui Diarra amesepa na hati safi kwenye mchezo huo akifikisha jumla ya hati safi 15 tofauti moja na kinara ambaye ni Moussa Camara kipa namba moja wa Simba SC.

Mabao ya Yanga SC yalifungwa na Aziz Ki dakika ya 26, Prince Dube dakika ya 30 na Maxi Nzengeli dakika ya 72. Ushindi huo unaipa Yanga SC pointi tatu wakifikisha jumla pointi 73 kibindoni nafasi ya kwanza kwenye msimamo.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.