YANGA SC: TUMEBAKIWA NA MECHI MBILI TU ZA LIGI

UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa umebakiwa na mechi mbili za Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25 mara baada ya kucheza dhidi ya Namungo FC, Mei 3 2025.

Katika mchezo huo ambao unakuwa ni wa 27 kwa Yanga SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 3-0 Namungo FC pointi tatu zikibaki Jangwani.

Kila mzunguko kuna michezo 15 kwa timu ambapo Yanga hilo ilikamilisha mzunguko wa kwanza na mzunguko wa pili ni mechi 12 imecheza nakufanya icheza jumla ya mechi 27 zikibaki mechi tatu.

Mechi ya tatu ni dhidi ya watani zao wa Jadi Simba SC ambayo awali ilitarajiwa kuchezwa Machi 8 2025 ikaahirishwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB), wametoa ratiba ambayo inaonyesha kuwa mchezo huo wa Yanga SC vs Simba SC ambao ni namba 184 utachezwa Juni 15 2025.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga SC amesema kuwa kwa mujibu wa ratiba ambayo wanayo wao wamebakiwa na mechi mbili za ligi na nyingine ni kwenye CRDB Federation Cup.

“Tuna mechi mbili ambazo zimebaki kwenye ligi ambapo kuna mchezo dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji baada ya hapo tutakuwa tumemaliza mechi za ligi kwa upande wetu na kile ambacho tunakitambua sisi.

“Kwa upande wa CRDB Federation Cup tuna mchezo dhidi ya JKT Tanzania ambao ni nusu fainali ikiwa tutapita hapo tutakuwa na mchezo mmoja wa fainali hivyo itafanya kwa msimu wa 2024/25 tuwe na mechi nne ambazo zimebaki.”