YANGA SC 3-0 NAMUNGO FC, JASHO ILIVUJA DAKIKA 90

MCHEZO wa mzunguko wa pili uliochezwa Uwanja wa KMC Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga SC 3-0 Namungo FC huku jasho likiwavuja wachezaji kwenye kutimiza majukumu yao.

Hapa tunakuletea baadhi ya walichokifanya wachezaji wa timu zote mbili katika kutimiza majukumu yao ilikuwa namna hii:-

Djigui Diarra

 Djigui Diara alisepa na dakika 90 na aliokoa hatari dakika ya 9 kutoka kwenye miguu ya Fabrince wa Namungo FC ambaye alipata maumivu dakika ya 35 alikwama kukamilisha dakika 90.

Nahimana

Kipa wa Namungo FC, Jonathan Nahimana ambaye alianza kikosi cha kwanza licha ya kutunguliwa mabao matatu, mikono yake ilikuwa kwenye kazi kubwa aliokoa hatari dakika ya 19, 20, 24, 31, 38 double save dakika ya 45. Kipindi cha pili aliendelea kazi yake langoni akiokoa hatari dakika ya 46, 47, 67, 70, 90.

Muda

Mudathir Yahya, kiungo wa Yanga SC alitoa pasi fupi dakika ya 40 aliokoa hatari dakika ya 43 alipiga krosi dakika ya 61 alikomba dakika 66 nafasi yake ilichukuliwa na Aziz Andambwile.

Prince Dube

Prince Dube mshambuliaji wa Yanga SC alipachika bao moja dakika ya 30 alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 45, alicheza faulo dakika ya 46. Bao hilo mbele ya Namungo FC linamfanya afikishe mabao 13. Aligotea dakika ya 78 nafasi yake aliingia Kennedy Musonda.

Kibabage

Nickson Kibabage wa Yanga SC alitoa pasi dakika ya 8, alipewa majukumu ya kurusha dakika ya 16 alicheza faulo dakika ya 4, alipiga krosi dakika ya 46

Mzize

Clement Mzize mshambuliaji wa Yanga SC cheza faulo dk 3, otea dk 4, 9, chezewa faulo dk 31 na Kabunda, alicheza faulo dakika ya 67, aligotea dakika ya 78 nafasi yake aliingia Dennis Nkane.

Job

Dickson Job aliokoa hatari dakika ya 6, 14 alikomba dakika zote 90.

Nondo

Bakari Nondo, aliokoa hatari dakika ya 3, 4, 8, 18, 40 alichezewa faulo dakika ya 11, alicheza faulo dakika ya 35 kwa Fabrince na alionyeshwa kadi ya  njano dakika ya 35, aliokoa hatari dakika ya 55.

Aziz Ki

Aziz Ki alipiga faulo dakika ya 6, alipiga kona dakika ya 16, 19, alifunga bao dakika ya 26 kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18 alipiga shuti lililolenga lango dakika ya 31, alipiga faulo dakika ya 45,58 alikomba dakika 60 nafasi yake ilichukuliwa na Clatous Chama.

Maxi Nzengeli

Maxi Nzengeli alicheza faulo dakika ya 6, alipiga kona dakika ya 25, 45, alitoa pasi ya bao dakika ya 26 alimpa Aziz Ki, alikokota mpira dakika ya 40 alipiga kona dakika ya 70, alipachika bao moja kwa mguu wa kushoto akiwa ndani ya 18.

Kibwana Shomari

Kibwana Shomari alipewa majukumu ya kurusha dakika ya 14, 20, aliokoa hatari dakika ya 19, 42 alitoa pasi ya bao dakika ya 30 alimpa Dube. Kibwana Shomari aligotea dakika ya 45 nafasi yake ilichukuliwa na Israel Mwenda, aliyetoa pasi ya bao kwa Maxi.

Saleh Karabaka

Saleh Karabaka alichezewa faulo dakika ya 10, alicheza faulo dakika ya 11, alipiga kona dakika ya 23.

Fabrice alipiga shuti ambalo lililenga lango dakika ya 9 alichezewa faulo dakika ya 36 na Nondo alikwama kukamilisha dakika 90 nafasi yake ilichukuliwa na Meddie Kagere.

Hassan Kabunda

Hassan Kabuda alichezewa faulo na Mzize dakika ya 3, 22, Kabuda aligotea dakika ya 50 nafasi yake ikachukuliwa na Jacob Masawe.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.