WINGA wa Simba SC ambaye ni chaguo la kwanza ndani ya kikosi hicho kinachotarajiwa kucheza mchezo wa hatua ya fainali dhidi ya RS Berkane, Mei 17 2025 anatajwa kuwa kwenye rada za Yanga SC kutokana na taarifa kueleza kuwa yupo hapo kwa mkopo.
Baada ya taarifa hizo kuenea uongozi wa Simba SC umebainisha kuwa hakuna ukweli kuhusu jambo hilo kwa kuwa mchezaji huyo bado ana mkataba na timu hiyo.
Mpanzu kwenye mechi za ligi na anga za kimataifa amekuwa kwenye mwendo mzuri jambo ambalo limeongeza thamani yake katika kikosi cha kwanza na kuwapa wapinzani wao ugumu kwenye kutafuta matokeo.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa wanatambua yote ambayo yanaendelea kutokana na baadhi ya timu kufuatilia kupata saini ya Ellie Mpanzu.
“Wanahangaika ninaona na ninajua kwamba watashindwa kupata kile ambacho wanahitaji.Mchezaji Mpanzu ni mali ya Simba SC na ana mkataba na timu hivyo waache wahangaike kwa namna yoyote ile.
“Kazi yetu kuwapa burudani mashabiki na wale ambao wanahitaji kupata saini yake watahangaika bila mafanikio kwa kuwa mchezaji ni mali yetu ana mkataba wa miaka miwili.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.