AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa kadri wapinzani wao wanavyozidi kuchelewa kucheza na timu hiyo watakutana na wachezaji wakiwa kwenye ubora mkubwa zaidi ya sasa.
Mchezo unaofuata kwa Simba SC kwenye ligi ni dhidi ya Yanga SC unaotarajiwa kuchezwa Juni 15 2025 baada ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) kupanga tarehe mpya huku Yanga SC wakibainisha kuwa hawatacheza mchezo huo.
Ally amesema: “Kwa kadri ambavyo Simba SC inacheza halafu kunakuwa na timu inakawia kuleta timu uwanjani itakutana na wachezaji wakiwa kwenye ubora mkubwa zaidi hao akina Mpanzu, Mutale watakuwa hawakamatiki.”