MATAJIRI wa Dar, Azam FC wamekomba pointi tatu mazima kwa kupata ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Mei 13 2025, Azam Complex.
Lusajo Mwaikenda alifungua ukurasa dakika ya 6, Abdul Sopu bao la pili dakika ya 17, Gibril Sillah bao la tatu dakika ya 20, Nasor Saadun dakika ya 27 na kamba ya tano ni mali ya Frank Tiesse dakika ya 55.
Lusajo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo baada ya dakika 90 ambapo Azam FC walipeleka kilio kwa wakulima wazabibu.
Vita yao kwenye nafasi ya tatu inazidi kupamba moto ambapo washindano wao Singida Black Stars wamecheza mechi 27 wana mchezo mmoja mkononi kufikisha mechi 28.
Kete yao ijayo kwa Singida Black Stars ni dhidi ya Simba SC mchezo unaotarajiwa kuchezwa Mei 28 Uwanja wa KMC Complex kwenye msako wa pointi tatu muhimu.
Singida Black Stars kibindoni ina pointi 53 baada ya mechi 27 huku Azam FC ikiwa nafasi ya tatu na pointi 57 baada ya mechi 28.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.