MILOUD Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga SC amesema kuwa wapo madhubuti kuwakabili wapinzani wao Namungo FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili 2024/25.
Ni mchezo wa mzunguko wa pili unaotarajiwa kuchezwa Mei 13 2025, Uwanja wa KMC Complex saa 10:15 kwa wanaume 22 kupambania pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.
Novemba 30 2025 Uwanja wa Majaliwa ulisoma Namungo 0-2 Yanga SC hivyo mchezo wa leo itakuwa ni kisasi kwa Namungo FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda kusaka pointi tatu huku Yanga SC wakilinda rekodi yao.
Kwenye msimamo wa ligi, Yanga SC ni vinara wakiwa na pointi 70 baada ya kucheza mechi 26, ushindi ni kwenye mechi 23, sare moja na kupoteza mechi mbili. Namungo FC nafasi ya 10 wakiwa na pointi 31 kibindoni.
Kocha Miloud amebainisha kuwa maandalizi yao yapo vizuri kwa ajili ya kukabiliana na wapinzani wao Namungo FC kwenye mchezo wao wa ligi wakiwa tayari kupata matokeo kutokana na utayari wa wachezaji.
“Tumejiandaa vizuri sana kuelekea mchezo wetu, wachezaji wote wana morali ya kutosha kukabiliana na Namungo FC. Tunajua wazi kuwa Namungo wanautaka mchezo huu kuhakikisha wanapata alama muhimu kwao. Tuna muda mrefu bila mechi ya ushindani hivyo tutacheza kwa umakini mkubwa.
“Lengo letu kuu ni moja tu, kushinda kila mechi ambayo ipo mbele yetu. Tunahitaji kuwa mabingwa msimu huu na hilo lipo wazi. Nawaheshimu Namungo, nafahamu wana timu nzuri lakini kwetu sisi ni mchezo muhimu wa kushinda, hatupaswi kabisa kudondosha alama tena ukizingatia tupo nyumbani. Alama tatu kwetu ni muhimu mno. Nina furaha baadhi ya wachezaji wangu muhimu wote wamerejea kwenye kikosi, hivyo nina kikosi Madhubuti.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.