RATIB LIGI KUU BARA MEI 13 2025

MECHI za Ligi Kuu Tanzania Bara zinatarajiwa kuendelea ambapo ni mzunguko wa pili leo Mei 13 2025 kuna timu zitakuwa uwanjani katika msako wa pointi tatu muhimu.

Wakati Mei 12 2025, ubao wa Uwanja wa Kaitaba ukisoma Kagera Sugar 0-1 Mashujaa FC, Tanzania Prisons 2-1 Coastal Union, kuna mwendelezo mwingine itakuwa leo.

Ratiba ipo namna hii:-

JKT Tanzania iliyo nafasi ya 8 ikiwa na pointi 32 baada ya mechi 27 itakabiriana na Fountain Gate iliyo nafasi ya 13 na pointi 29 (Saa 8:00 Mchana).

KenGold iliyo nafasi ya 16 na pointi 16 itakabiliana na Pamba FC iliyo nafasi ya 14 na pointi 27 (Saa 10:15 Alasiri)

Yanga iliyo nafasi ya kwanza na pointi 70 itakawakabili Namungo FC iliyo nafasi ya 10 na pointi 31(Saa 10:15 Alasiri)

Azam FC iliyo nafasi ya tatu kwenye msimamo na pointi 54 itakabiliana na Dodoma Jiji iliyo nafasi ya 6 na pointi 34. (Saa 1:00 Usiku)

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.