BAADA ya kupoteza mchezo wa mzunguko wa kwanza kwenye Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora uliochezwa Novemba 30 2024 ubao wa Uwanja wa Majaliwa ukasoma Namungo 0-2 Yanga SC, Namungo FC wameweka wazi kuwa watawakabili wapinzani wao kwa mbinu tofauti kupata matokeo chanya,
Mei 13 2025, Namungo FC inatarajiwa kushuka Uwanja wa KMC Complex kwenye msako wa pointi tatu ikiwa chini ya Kocha Mkuu Juma Mgunda na Mei 12 2025 Namungo FC walifanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya kuwakabili wapinzani wao Yanga SC.
Kocha msaidizi wa Namungo FC, Ngawina Ngawina amesema kuwa wanawaheshimu wapinzani wao Yanga SC kutokana na kuwa na timu imara yenye wachezaji wazuri hivyo wataingia kwa tahadhari kutafuta matokeo.
“Mchezo wetu dhidi ya Yanga tunaamini utakuwa mchezo mzuri tunawaheshimu Yanga wana timu nzuri na wachezaji wazuri pia sisi Namungo tumekuwa na muda mzuri wa kujiandaa kwasababu kila mchezo una mbinu yake ya kucheza kulingana na mpinzani tunayeenda kukutana nae.
“Tumekuwa na muda mrefu wa maandalizi yuna imani tutafanya vizuri kwenye mchezo wetu dhidi ya Yanga SC, tutaingia kwa tahadhari ili kupata matokeo mazuri kwani mpinzani wetu sio wakumbeza.”
Kwenye msimamo Namungo FC ipo nafasi ya 10 imecheza mechi 27 ushindi ni kwenye mechi 8, sare 7 ikipoteza mechi 12 huku safu ya ushambuliaji ikitupia mabao 23 kibindoni ni pointi 31. Inakutana na Yanga SC iliyo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 26 pointi 70 safu ya ushambuliaji imetupia mabao 68.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.