USHINDI wa mabao 5-1 ambao wameupata Simba SC kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Pamba Jiji, Mei 8 2025 unawafanya wakamilishe dakika 270 katika mechi tatu za viporo kuvuna pointi tatu mazima kwenye mechi zao.
Mchezo wa kwanza wa kiporo kwa Simba SC ilikuwa Mei 2 2025, ubao wa Uwanja wa KMC Complex ulisoma Simba SC 2-1 Mashujaa FC, Mei 5 2025, JKT Tanzania 0-1 Simba SC na Mei 8 2025, Simba 5-1 Pamba Jiji.
Moussa Camara, kipa namba moja wa Simba SC kwenye mechi tatu katunguliwa mabao mawili ndani ya dakika 270 na kumfanya abaki na hati zake safi 16 baada ya kukaa langoni kwenye mechi 23.
Katika mchezo dhidi ya Pamba Jiji, kiungo mshambuliaji Jean Ahoua alifunga hat trick dakika ya 16 kwa pigo la penalti iliyosababishwa na Joshua Mutale bao la pili Ahoua alipachika dakika ya 37 na bao la tatu dakika ya 47 kwa pigo la kichwa.
Mabao mawil yalifungwa na mshambuliaji Leonel Ateba dakika ya 80 akiwa ndani ya 18 na bao la tano Ateba kafunga dakika ya 84.
Pamba Jiji walitumia dakika mbili kupata bao la kufutia machozi kupitia kwa mshambuliaji Mathew Tegisi ambaye alipachika bao kwa Pamba Jiji dakika ya 86.
Pamba Jiji inabaki nafasi ya 13 kwenye msimamo baada ya kucheza mechi 27 ikipata ushindi kwenye mechi 6, sare 9 huku ikipoteza mechi 12 ni pointi 27 wanazo kibindoni msimu wa 2024/25.
Simba SC ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 66 baada ya mechi 25 ikipata ushindi kwenye mechi 21, sare tatu na ilipoteza mchezo mmoja ndani ya uwanja.
Mwamuzi Shomari Lawi dakika ya 90 alimuonyesha kadi nyekundu mchezaji wa Pamba Jiji Hamad Majimengi dakika ya 90.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.